UTAANGULIZI
VIGEZO MUHIMU KATIKA UCHAMBUZI WA TAMTHILIA HII
JALADA LA KIFUNGANJIA
Jalada ni sehemu iliyoko juu ya kitabu .Huwa ni mambo yaliyo muhutasari wa kile msomaji
anatarajia ndani.Jalada huwa kuwili yaaani jalada la mbele na Jalada la nyuma.Rangi za michoro
na maandishi huwa ni vipengele muhimju katika uchambuzi.
Jalada la tamthilia hii kwenye upande wa mbele limechorwa; Mwanga mkuu wa rangi ya
manjano unaochomoza kutoka upande wa magharibi ambapo tunapata picha hafifu ya mandhari
ya upande.Mwingine wa mashariki.
Vilima viwili vinaoneka huku vikiwa vimetenganishwa na njia kuu.Upande wa magharibi
kwenye jalada hili umegubikwa na giza hafifu (kuna udunifu wa mwanga).Kwenye uesi wa
rangi(Giza) tunaona vizuizi na pia picha iliyokaa sawia na binadamu; nusu mnyama
aliyesimama.Mkono wake unaashiria.
Kwenye jalada la nyuma mwandishi Daniel Okello anaelezea kuhusu yaliyomo kwenye
tamthilia hii kinagaubaga.
ANWANI YA TAMTHILIA
Kifunganjia ni kifaa au kitu kinachozuia mapito (njia).
Katika tamthilia hii VIZUIZI katika maeneo ainati vimesawiriwa kama VIFUNGANJIA,
wakiwemo wahusika Wanaokumbwa na matatizo katika mandhari tofauti.
Kwa mfano;
1. Rajua anaonekana kuwa kizuizi anapojaribu kukemea matumizi ya madawa ya kulevya
2. Mtumishi Matata (uk74) anaonekana kuwa kizuizi cha maendeleo kwa kujaribu kumpa
hongo Rajua ili awache siasa na ampe nafasi kwa ofisi yake.
3. Kuzingira ghala ili wanakijiji wasione ni mojawapo pia ya kizuizi.
4. Vidude vya mama Rajua vinawazuia vijana kufanya kazi.
5. Viongozi wabaya ni vifunganjia kwa maendeleo ya wanabakunja.
DHAMIRA YA MWANDISHI/LENGO/MINTARAFU/KUSUDI
o Dhamira huelezwa kama lengo au shabaha ya mwandishi katika kazi ya fasihi.
,Mwandishi wa tamthilia ya Kifunganjia anadhamiria.
Kutuonyesha kuwa ili kujenga jamii mpya, mapindunzi ni muhimu na ni lazima
Kutuonyesha masaibu ya pombe katika jamii
Kutuonyesha jinsi uongonzi wa jamii unadhuru jamii
Kutuonyesha uozo uliopo katika dini ukitekeleza na wanaodai kuwa viongozi.
MTIRIKO WA MAONYESHO
TENDO LA KWANZA
ONYESHO LA I
Ni asubuhi katika uwanja mawe yametawanyika huko yakiwa yamezingira ghala
Watu waliovalia suti wanaonekana wakisinikizwa na askari waliovalia sare.
Sauti ya ushairi inasikika kuhusu ghala.
Watu wale wawili wenye hamaki wanaondoka mahali pale.
Tembo na komba wanaingia wakiwa wamebepa pombe mkononi vile vile wanasikika
wakilalamika kuhusu ghala lisillojaa huko paka panya wakizingiziwa .Ghafla
wanapowaona askari wanakimbia na kuificha
ONYESHO LA II
Tembo na Komba wangali wapo pale wamejificha.Rajua anatokea huko katika
uzungumzi nafsi.
Rajua anajipa moyo kuwa anaweza kubadilisha hali ilivyo katika jamii;anaweza
kuboresha mazingira na mashamba anaamin kuwa hatua ya kwanza ni kutenga ukweli na
uongo.(uk16)
Mzee anatokea na Rajua anamhoji kwa upezi, mahojiano hayo yanatupa chanzo cha
panya na mchwa wanaowakabili wanakijiji.Baada ya mahojiano wote wanaondoka.
ONYESHO LA III
Katika onyesho hili Tembo na Komba wanaonekana wakiwa walevi karibu na ghala .
Onyesho hili linazungumzia kuhusu fikira za wanabukunja kumhusu Mwanamapinduzi
Rajua .
Licha ya matatizo waliyo nayo tunaona kuwa kuna wale wanaomdunisha na kumkejeli
Rajua
(uk24).
Vile vile onyesho ili linaangazia mchango wa mwanamke katika familia pale ambapo
Tembo wanaacha familia zao bila kujali.
, TENDO LA PILI
ONYESHO LA I
Onyesho hili linaanza kwenye nyumba nyuma ya Mama Shari mwendo wa alasiri.
Shari wanapatana na mpenzi wake Rajua.Shari na Rajua wanazungumzia kuhu michezo
ya kuigiza na pia utafiti maabarani.
Punde si punde Rajua na Shari wanafumanishwa na mamake Shari mwenye
hamaki.Mama Shari anakashifu vikali uhusiano wa wawili hawa na pia anamduninisha
Rajua.
Shari anakasirika na kuondoka nyumbani.
ONYESHO LA II
Onyesho hili linaanza kwa kina shari huku mamake Shari akimkaribisha bwanake
(KOMBA) kwa heshima kuu (uk36) anampokea na kumtia mume wake moyo kwa hali
ngumu wanayopitia.
Kombo analamika kuhusu chakula duni.Mamake anamwazia shari ilhali Komba
anamtetea mwanake.Hali ya Shari inazua ugomvi baina ya wazazi wake.Komba
anaondoka kwa kishindo.
ONYESHO LA III
Nyumba ni ile ya kina Shari Mtumishi anakaribishwa ndani na mama Shari.Mtumishi
amekuja kumuharifu Shari kuhu mambo ya maabarani.
Shari anaomba Baraka na wosia kutoka kwa mtumishi.Mtumimishi anamuonya Shari
dhidi ya roho chafu maabarani
Mtumishi anamzawdi Shari simu baada ya maombi.Mtumishi na Shari wanaondoka.
ONYESHO LA IV
Giza linapoelekea kuingia Shari na Zandiki wanapatana na kuanza kufanyiana utani
kuhusu urembo wao
Na safari yao ya mapenzi.Baada majisifu wanahofya giza kuingia wote wanaondoka na
kuelekea sehemu mbili tofauti.
ONYESHO LA V
Onyesho ili linaanza maabarani Zandiki na Shari wamekaa viti vya nyuma
wakibonyezabonyeza simu zao
Wanamsikiza mtaalamu kwenye maabara.Baada ya swali kutoka kwa mwanafunzi
(Waridi) na pongenzi mtaalam anamkaribisha Rajua atoe historia ya Bakunja.
Zandiki na Shari wanaonekana kupuuza mafunzo ya Rajua.
Rajua anaelezea kwa ukakamavu kuhusu ghala na matumaini ya wanabakunja.