100% satisfaction guarantee Immediately available after payment Both online and in PDF No strings attached 4.2 TrustPilot
logo-home
Summary

Summary FASIHI SIMULIZI NOTES

Rating
-
Sold
-
Pages
47
Uploaded on
28-11-2022
Written in
2022/2023

Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kuwasilisha ujumbe unaomhusu binadamu. Sanaa ni ufundi wa kuwasilisha fikra na hisia za binadamu kama vile maneno, maandishi, uchoraji, uchongaji, ufinyanzi n.k. Fasihi simulizi ni sanaa kwa vile: a) Huwasilisha ujumbe kuhusu binadamu kuhusu utamaduni na uchumi. b) Huwa na umbo mahsusi k.m. hadithi huwa na mwanzo, kati na mwisho na mashairi huwa na beti, mishororo, n.k. c) Hutumia lugha kwa ufundi k.v. ya kitamathali. d) Husawiri mandhari/mazingira mahsusi kwa ufundi mkubwa. e) Hujenga wahusika kwa ustadi mkuu ili kusawiri tabia za watu katika jamii. Tofauti Kati ya Fasihi na Sanaa Nyingine fasihi sanaa nyingine  Kutumia lugha  Sanaa tendi  Kutumia wahusika kuwasilisha maudhui  Kutumia maudhui na fani kuwasilisha ujumbe  Kujikita katika mazingira na wakati maalum  Kutotumia lugha  Si tendi  Hutumia maumbo kumithilisha watu  Kutumia maumbo na sura za vitu  Hazijikiti katika muktadha na wakati maalum. Aina/makundi ya fasihi a) Fasihi simulizi  Fasihi inayowasiolishwa kwa njia ya mdomo. b) Fasihi andishi  Fasihi inayowasilishwa kwa njia ya maandishi. Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi/sifa za fasihi simulizi/zinazofanya utanzu uwe wa fasihi simulizi a) Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo ilhali fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi. b) Fasihi simulizi huhifadhiwa akilini ilhali fasihi aandishi huhifadhiwa kwa maandishi. c) Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mtu binafsi/mwandishi. d) Fasihi simulizi ina wahusika wa kila aina k.v binadamu, wanyama na ndege, mazimwi na majitu, miungu, mizimu, mashetani na vitu visivyo na uhai k.v. mawe na miti ilhali fasihi andishi ina wahusika binadamu kwa kiasi kikubwa. e) Fasihi simulizi ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishi. f) Uwasilishaji wa fasihi simulizi huweza kuandamana na utendaji k.v matumizi ya ishara, nyimbo, makofi, kuimba, kubeba zana katika majigambo n.k ilhali ule wa fasihi andishi hauandamani na utendaji isipokuwa inapowasilishwa mbele ya hadhira. g) Fasihi simulizi huwasilishwa mbele ya hadhira ilhali fasihi andishi si lazima iwasilishwe mbele ya hadhira. h) Fasihi simulizi huwasilishwa mahali maalum k.v jandoni, matangani, arusini, n.k ilhali fasihi andishi haina mahali maalum. i) Fasihi simulizi huandamana na shughuli fulani ya kitamaduni ilhali fasihi andishi haiandamani na shughuli ya kitamaduni. 3 j) Fasihi andishi huhitaji muda kutunga ilhali baadhi ya fasihi simulizi huzuka papo hapo k.m. semi, maigambo. k) Fasihi simulizi ina uwezo mkubwa wa kubadilishwa na fanani anapowasilisha ufaraguzi) bali fasihi andishi haibadiliki isipokuwa mwandishi aiandike upya. l) Fasihi simulizi ina historia ndefu kuliko fasihi andishi kwa kuwepo tangu mwanzo wa maisha ya binadamu m) Fasihi simulizi huwasilishwa wakati maalum k.v. usiku, kipindi fulani cha mwaka ilhali andishi haina wakati maalum.  Tofauti kati ya hadhira n) Hadhira ya fasihi simulizi huweza kuwasiliana moja kwa moja na mwasilishaji ilhali ile ya fasihi simulizi sio lazima iwasiliane na mwandishi. o) Hadhira huchangia katika uwasilishaji wa fasihi simulizi k.v kwa kuimba, kupiga makofi n.k (hadhira tendi/hai) ilhali hadhira ya fasihi andishi haichangii katika uandishi. p) Hadhira ya fasihi simulizi huonana na mwasilishaji ilhali ile ya fasihi andishi si lazima ionane na mwandishi. q) Hadhira ya fasihi simulizi ni kubwa kuliko ile ya fasihi andishi kwani huhusisha hata wasiojua kusoma na kuandika. r) Hadhira ya fasihi simulizi ni hai yaani inajulikana na fanani ilhali ile ya fasihi simulizi si hai yaani haijulikani na mwandishi. s) Hadhira ya fasihi simulizi hainunui kazi ilhali ile ya fasihi andishi hununua kazi. t) Hadhira ya fasihi simulizi yaweza kumiliki kazi ya fanani lakini ile ya fasihi andishi haiwezi kumiliki kazi ya mwandishi. u) Hadhira ya fasihi simulizi huchagua kwa kulenga watu wa rika fulani lakini ile ya fasihi andishi hailengi watu wa rika yoyote. Jinsi Fasihi Simulizi na Andishi Zinavyofanana a) Zote mbili hushughulikia masuala yanayohusu maisha ya binadamu. b) Zote mbili Hutumia lugha kwa ubunifu kuwasilisha maudhui. c) Zote mbili huwa na vipengele viwili vikuu, maudhui na fani (jumla ya mbinu msanii alizotumia kuwasilisha maudhui). d) Zote mbili majukumu sawa k.v. kuburudisha, kuadilisha, kuhifadhi na kuendeleza utamaduni, n.k. e) Zote mbili zina utendaji-pale tamthilia na riwaya zinapoigizwa. f) Zote mbili huzaliwa, hukua na hufa kutegemea mabadiliko ya wakati. g) Zote mbili huwa na wawasilishaji-fanani k.m. mtambaji/mganaji au manju/yeli katika fasihi simulizi na mwandishi upande wa fasihi andishi . h) Fasihi simulizi imekopa tanzu za fasihi simulizi k.v. methali, mashairi, n.k. Majukumu ya Fasihi Simulizi/Umuhimu wa Kufunza Fasihi Simulizi Katika Shule za Upili a) Kuburudisha-kustarehesha, kufurahisha, kuchangamsha, kutuliza, kusisimua na kupumbaza akili na kiwiliwili - nyimbo, hadithi, vitendawili b) Kufunza maadili kwa wanajamii kwa kuwahimiza kuiga sifa chanya na kukataa sifa hasi za wahusika. c) Kukuza uwezo wa kufikiri/kudadisi k.m vitendawili na chemshabongo. d) Kufariji k.m mbolezi na methali k.m. ‘Baada ya dhiki faraja’. e) Vipengele vya fasihi simulizi k.v mashairi, nyimbo, nahau, hutumiwa katika uandishi wa fasihi andishi. f) Kuhifadhi historia ya jamii k.m. mighani, visaviini, mapisi, tarihi n.k. g) Kukejeli tabia zinazokiuka matarajio ya jamii k.v soga, methali, n.k. h) Kuendeleza tamaduni za jamii kwani husawiri imani na desturi za jamii. k.v kitendawili ‘Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini siwezi kulichuma.’ - Mtu hawezi kumwoa dadake. i) Kuunganisha watu pamoja kwa kuwajumuisha pamoja wakati wa ngoma, kuimba, utambaji, n.k. j) Kukuza lugha k.v. misimu inapokita kimatumizi na kujumuishwa katika lugha sanifu. k) Kukuza uwezo wa kutumia lugha kadiri mtu anapoendelea kuwasilisha k.v. hotuba, vitanza ndimi husaidia kuboresha matamshi na kutofautisha maana za maneno. l) Kuza uwezo wa kubuni k.v. malumano ya utani, vitanza, ndimi ngonjera, n.k. 4 m) Kukuza uzalendo kwa kufanya wanajamii kuonea fahari jamii zao na kuiga mashujaa au watu waliotendea jamii makuu. n) Kuonya na kutahadharisha wanajamii dhidi ya tabia hasi k.v. ulafi, uchoyo, n.k. Sababu za Ufaraguzi/Kubadilika kwa Fasihi Simulizi a) Kuwasilishwa vibaya. b) Fanani kusahau na kubadilisha yaliyomo na mtiririko. c) Kubadilisha ili kukidhi mahitaji ya hadhira k.m. umri na uelewa wao- kutumia lugha nyepesi kwa watoto na pevu kwa watu wazima. d) Mabadiliko ya mandhari/mazingira-vitu vilivyo katika mazingira halisi kukosekana katika mazingira ya usimulizi na msimulizi kutumia vitu katika mazingira yake vinavyokaribiana navyo. e) Kutoeleweka na hivyo kuhifadhiwa vibaya. f) Mabadiliko ya wakati k.m kitendawili cha wakati wa mkoloni kutumia mzungu na cha wakati wa mwarabu kutumia mwarabu na maana ni ile ile-Mzungu/mwarabu amesimama kwa mguu mmoja-mwavuli. g) Mabadiliko ya falsafa ya vizazi na maingiliano katika jamii kusababisha kurithisha tu yale ambayo ni muhimu na kuacha mengine. h) Kila fanani huwa na mtindo wake wa kuwasilisha/kisanii. i) Ubunifu wa fanani ili uwasilishaji uweze kuvutia saidi na uwezo wake wa lugha. j) Teknolojia kusababisha kuhifadhiwa na hivyo kuiua. Wahusika katika Fasihi Simulizi  Wahusika ni viumbe wa sanaa ambao hutumiwa katika kazi ya fasihi kuwasilisha maswala mbalimbali. a) Fanani-anayetunga na kuwasilisha fasihi simulizi. b) Hadhira-kusikiliza, kutazama, kushiriki wa kuimba, kuuliza maswali, kutegua vitendawili, kupiga makofi, n.k. kuna aina mbili za hadhira: (i) hadhira tendi/hai na (ii) hadhira tuli. c) Wanyama-wanaofanya kama binadamu na kuwakilisha sifa kama vile ujanja, ulaghai, tamaa na ujinga na wanaobakia wanyama tu. d) Binadamu e) Mazimwi na majitu-viumbe vyenye matendo na maumbile ya kutisha kama vile jicho moja, vichwa viwili au zaidi, nusu mtu na nusu myama, wenye tamaa iliyokithiri ya kuweza kumeza kila kitu, kuhifadhi na kutunza binadamu ananyoyapendeza. f) Wahusika vitu (visivyo na uhai) mawe, miti, vijaluba, vibuyu-hutumiwa kuibua imani za kidini. g) Mizimu-roho za waliokufa-hutembea, hula na huathiri binadamu. h) Miungu-viumbe vyenye uwezo mkubwa dhidi ya binadamu k.m. katika mighani na visasili. Njia za Kukusanya Fasihi Simulizi a) Kuchunza/utazamaji  Kutazama kwa makini yanayotokea na kuandika. Umuhimu/ubora/uzuri a) Kupata habari za kutegemewa na kuaminika. b) Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k. c) Ni njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika d) Kuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k. e) Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji Udhaifu a) Shida ya mawasiliano. b) Ugeni wa mtafiti kusababisha washiriki kumshuku na kusitisha uwasilishaji c) Ghali kwa kumbidi mtafiti kusafiri d) huhitaji muda mrefu b) Kusikiliza wasanii wakiwasilisha tungo zao. Umuhimu a) Kuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k. b) Kupata habari za kutegemewa na kuaminika. c) Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k. 5 d) Kikwazo cha mawasiliano-Si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika. e) Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji. Udhaifu a) Shida ya mawasiliano-Si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika. b) Huhitaji muda mrefu-kusafiri na kusikiliza. c) Ugeni wa mtafiti kusababisha washiriki kutowasilisha ipasavyo. d) Ghali kwa gharama ya usafiri. c) Mahojiano

Show more Read less
Institution
KISWAHILI
Course
KISWAHILI











Whoops! We can’t load your doc right now. Try again or contact support.

Written for

Institution
KISWAHILI
Course
KISWAHILI

Document information

Uploaded on
November 28, 2022
Number of pages
47
Written in
2022/2023
Type
Summary

Subjects

  • maandishi
  • uchoraji
  • uchongaji

Content preview

1 FASIHI SIMULIZI NOTES Carefully compiled the Smart way Compiled by Donold OTHER RESOURCES  All Subjects Notes (Form1, 2, 3 & 4)  Schemes of Work (Latest & Up to date)  Revision Booklets (Carefully compiled)  Exams (Opener, Mid-Term & End-Term)  All KASNEB Notes  Quality Set -Books Acted Videos WHATSAPP/CALL: 0718488005 or 0714930676 (MR. DONOLD M.N) 2 FASIHI SIMULIZI Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kuwasilisha ujumbe unaomhusu binadamu . Sanaa ni ufundi wa kuwasilisha fikra na hisia za binadamu kama vile maneno, maan dishi, uchoraji, uchongaji , ufinyanzi n.k. Fasihi simulizi ni sanaa kwa vile: a) Huwasilish a ujumbe kuhusu binadamu kuhusu utamaduni na uchumi. b) Huwa na umbo mahsusi k.m. hadithi huwa na mwanzo, kati na mwisho na mashairi huwa na beti, mishororo, n.k. c) Hutumia lugha kwa ufundi k.v. ya kitamathali. d) Husawiri mandhari/ mazingira mahsusi kwa ufundi mku bwa. e) Hujenga wahusika kwa ustadi mkuu ili kusawiri tabia za watu katika jamii. Tofauti Kati ya Fasihi na Sanaa Nyingine fasihi sanaa nyingine  Kutumia lugha  Sanaa tendi  Kutumia wahusika kuwasilisha maudhui  Kutumia maudhui na fani kuwasilisha ujumbe  Kujikit a katika mazingira na wakati maalum  Kutotumia lugha  Si tendi  Hutumia maumbo kumithilisha watu  Kutumia maumbo na sura za vitu  Hazi jikiti katika muktadha na wakati maalum. Aina/makundi y a fasihi a) Fasihi simulizi  Fasihi inayowasiolishwa kwa njia ya mdomo . b) Fasihi andishi  Fasihi inayowasilishwa kwa njia ya maandishi . Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi /sifa za fasihi simulizi/zinazofanya utanzu uwe wa fasihi simulizi a) Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo ilhali fasihi andishi huwasilishw a kwa njia ya maandishi . b) Fasihi simulizi huhifadhiwa akilini ilhali fasihi aandishi huhifadhiwa kwa maandishi . c) Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mtu binafsi/ mwandishi . d) Fasihi simulizi ina wahusika wa kila aina k.v binadamu, wanyam a na ndege , mazimwi na majitu, miungu, mizimu, mashetani na vitu visivyo na uhai k.v. mawe na miti ilhali fasihi andishi ina wahusika binadamu kwa kiasi kikubwa . e) Fasihi simulizi ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishi . f) Uwasilishaji wa fasihi simulizi huweza kuandamana na utendaji k.v matumizi ya ishara, nyimbo, makofi, kuimba , kubeba zana katika majigambo n.k ilhali ule wa fasihi andishi ha uandamani na utendaji isipokuwa inapowasilishwa mbele ya hadhira . g) Fasihi simulizi huwasilishwa mbele ya hadhira ilhali fasihi andishi si lazima iwasilishwe mbele ya hadhira . h) Fasihi simulizi huwasilishwa mahali maalum k.v jandoni, matangani , arusini, n.k ilhali fasihi andishi haina mahali maalum . i) Fasihi simulizi huandamana na shughuli fulani ya kitamaduni ilhali fasihi andishi haiandamani na shughuli ya kitamaduni . 3 j) Fasihi andishi huhitaji muda kutunga ilhali baadhi ya fasihi simulizi huzuka papo hapo k.m. semi , maigambo. k) Fasihi simulizi ina uwezo mkubwa wa kubadili shwa na fanani anapowasilisha ufaraguzi) bali fasihi andishi haibadiliki isipokuwa mwandishi aiandike upya . l) Fasihi simulizi i na historia ndefu kuliko fasihi andishi kwa kuwepo tangu mwanzo wa maisha ya binadamu m) Fasihi simulizi huwas ilishwa wakati maalum k.v. usiku , kipindi fulani cha mwaka ilhali andishi haina wakati maalum.  Tofauti kati ya hadhira n) Hadhira ya fasihi simulizi huweza kuwasiliana moja kwa moja na mwasilishaji ilhali ile ya fasihi simulizi sio lazima iwasiliane na mwandishi . o) Hadhira huchangia katika uwasilishaji wa fasihi simulizi k.v kwa kuimba, ku piga makofi n.k (hadhira tendi/hai) ilhali hadhira ya fasihi andishi haichangii katika uandishi . p) Hadhira ya fasihi simulizi huonana na mwasilishaji ilhali ile ya fasihi andishi si lazima ionane na mwandishi . q) Hadhira ya fasihi simulizi ni kubwa kuliko ile y a fasihi andish i kwani huhusisha hata wasiojua kusoma na kuandika . r) Hadhira ya fasihi simulizi ni hai yaani inajulikana na fanani ilhali ile ya fasihi simulizi si hai yaani haijulikani na mwandishi . s) Hadhira ya fasihi simulizi hainunui kazi ilhali ile ya fas ihi andishi hununua kazi . t) Hadhira ya fasihi simulizi yaweza kumiliki kazi ya fanani lakini ile ya fasihi andishi haiwezi kumiliki kazi ya mwandishi. u) Hadhira ya fasihi simulizi huc hagua kwa kulenga watu wa rika f ulani lakini ile ya fasihi andishi hailengi w atu wa rika yoyote . Jinsi Fasihi Simulizi na Andishi Zinavyofanana a) Zote mbili h ushughulikia masuala yanayohusu maisha ya binadamu. b) Zote mbili Hutumia lugha kwa ubunifu kuwasilisha maudhui . c) Zote mbili huwa na vipengele viwili vikuu, maudhui na fani ( jumla y a mbinu msanii alizotumia kuwasilisha maudhui ). d) Zote mbili m ajukumu sawa k.v. kuburudisha, kuadilisha, kuhifadhi na kuendeleza utamaduni, n.k. e) Zote mbili zina utendaji -pale tamt hilia na riwaya zinapoigizwa. f) Zote mbili huzaliwa, hukua na hufa kutegemea maba diliko ya wakati. g) Zote mbili huwa na wawasilishaji -fanani k.m. mtambaji/mganaji au manju/yeli katika fasihi simulizi na mwandishi upande wa fasihi andishi . h) Fasihi simulizi imekopa tanzu za fasihi simulizi k.v. methali, mashairi, n.k. Majukumu ya Fasihi Si mulizi /Umuhimu wa Kufunza Fasihi Simulizi Katika Shule za Upili a) Kuburudisha -kustarehesha, kufurah isha, kuchangamsha, kutuliza, kusisimua na kupumbaza akili na kiwiliwili - nyimbo, hadithi, vitenda wili b) Kufunza maadili kwa wanajamii kwa ku wahimiza k uiga sifa chanya na kuk ataa sifa hasi za wahusika . c) Kukuza uwezo wa kufikiri /kudadisi k.m vitendawili na chemshabongo. d) Kufariji k.m mbolezi na methali k.m . ‘Baada ya dhiki faraja’. e) Vipengele vya fasihi simulizi k.v mashairi, nyimbo, nahau, hutumiwa katika u andishi wa fasihi andishi. f) Kuhifadhi historia ya jamii k.m. mighani, visaviin i, mapisi, tarihi n.k. g) Kukejeli tabia zinazokiuka matarajio ya jamii k.v soga, methali, n.k. h) Kuendeleza tamaduni za jamii kwani husawiri imani na desturi za jamii. k.v kitendawili ‘Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini siwezi kulichuma .’ - Mtu hawezi kumwoa dadake. i) Kuunganisha watu pamoja kwa kuwa jumui sha pamoja wakati wa ngoma, kuimba, utambaji, n.k. j) Kukuza lugha k.v. misimu inapokita kimatumizi na kujumuishwa katika lugha san ifu. k) Kukuza uwezo wa kutumi a lugha kadiri mtu anapoendelea kuwasilisha k.v. hotuba, vitanza ndimi husaidia kuboresha matamshi na kutofautisha maana za maneno. l) Kuza uwezo wa kubuni k.v. malumano ya utani, vitanza, ndimi ngonjera, n.k. 4 m) Kukuza uzalendo kwa ku fanya wanajamii kuonea fahari jamii zao na kuiga mashujaa au watu waliotendea jamii makuu. n) Kuonya na kutahadharisha wanajamii dhidi ya tabi a hasi k.v. ulafi, uchoyo, n.k. Sababu za Ufaraguzi/ Kubadilika kwa Fasihi Simulizi a) Kuwasilishwa vibaya. b) Fanani kusaha u na kubadilisha yaliyomo na mtiririko. c) Kubadilisha ili kukidhi mahitaji ya hadhira k.m. umri na uelewa wao - kutumia lugha nyepesi kwa watoto na pevu kwa watu wazima. d) Mabadiliko ya mandhari/mazingira -vitu vilivyo katika mazingira halisi kukosekana katika mazingira ya usimulizi na msimulizi kutumia vitu katika mazingira yake vinavyokaribiana navyo. e) Kutoeleweka na hivyo kuhifadhiwa vibaya. f) Mabadiliko ya wakati k.m kitendawili cha wakati wa mkoloni kutumia mzungu na cha wakati wa mwarabu kutumia mwara bu na maa na ni ile ile -Mzungu/mwarabu amesimama kwa mguu mmoja -mwavuli. g) Mabadiliko ya falsafa ya vizazi na maingiliano katika jamii kusababisha kurithisha tu yale ambayo ni muhimu na kuacha mengine. h) Kila fanani huwa na mtindo wake wa kuwasilisha/kisanii . i) Ubuni fu wa fanani ili uwasilishaji uweze kuvutia saidi na uwezo wak e wa lugha. j) Teknolojia kusababisha kuhifadhiwa na hivyo kuiua . Wahusika katika Fasihi S imulizi  Wahusika ni viumbe wa sanaa ambao hutumiwa katika kazi ya fasihi kuwasilisha maswala mbalimbali. a) Fanani -anayetunga na kuwasilisha fasihi simulizi. b) Hadhira -kusikiliza, kutazama, kushiriki wa kuimba, kuuliza maswali, kutegua vitendawili, kupiga makofi, n.k. kuna aina mbili za hadhira: (i) hadhira tendi/hai na (ii) hadhira tuli. c) Wanyama -wanaofanya kama binadamu na kuwakilisha sifa kama vile ujanja, ulaghai, tamaa na ujinga na wanaobakia wanyama tu. d) Binadamu e) Mazimwi na majitu -viumbe vyenye matendo na maumbile ya kutisha kama vile jicho moja, vichwa viw ili au zaidi, nusu mtu na nusu myama, wenye tamaa iliyokithiri ya kuweza kumeza kila kitu, kuhifadhi na kutunza binadamu ana nyoyapendeza. f) Wahusika vitu (visivyo na uhai) mawe, miti, vijaluba, vibuyu -hutumiwa kuibua imani za kidini. g) Mizimu -roho za waliokufa -hutembea, hula na h uathiri binadamu. h) Miungu -viumbe vyenye uwe zo mkubwa dhidi ya binadamu k.m. katika mighani na visasili. Njia za Kukusanya Fasihi Simulizi a) Kuchunza /utazamaji  Kutazama kwa makini yanayotokea na kuandika . Umuhimu /ubora/uzuri a) Kupata habari za kutegemewa na kuaminika. b) Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k. c) Ni njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika d) Kuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k. e) Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji Udhaifu a) Shida ya mawasiliano. b) Ugeni wa mtafiti kusababisha washiriki kumshuku na kusitisha uwasilishaji c) Ghali kwa kumbidi mtafiti kusafiri d) huhitaji muda mrefu b) Kusikiliza wasanii wakiwasilisha tungo zao. Umuhimu a) Kuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k. b) Kupata habari za kutegemewa na kuaminika. c) Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k.

Get to know the seller

Seller avatar
Reputation scores are based on the amount of documents a seller has sold for a fee and the reviews they have received for those documents. There are three levels: Bronze, Silver and Gold. The better the reputation, the more your can rely on the quality of the sellers work.
SIRTHEA Chamberlain College Of Nursing
View profile
Follow You need to be logged in order to follow users or courses
Sold
24
Member since
3 year
Number of followers
24
Documents
611
Last sold
1 year ago
SAGACITY//////////////////////////////////////////

Hi,I'm Sirthea am expert on courses like;Nursing,Law,Psychology,Human Resource Management.I will be providing you with quality study materials everyday.I do ensure scolarly standards in my documents and i assure you a GOOD GRADE if you use my study resources.Please Don't forget to Review after using my resources.Thank You!

5.0

1 reviews

5
1
4
0
3
0
2
0
1
0

Recently viewed by you

Why students choose Stuvia

Created by fellow students, verified by reviews

Quality you can trust: written by students who passed their tests and reviewed by others who've used these notes.

Didn't get what you expected? Choose another document

No worries! You can instantly pick a different document that better fits what you're looking for.

Pay as you like, start learning right away

No subscription, no commitments. Pay the way you're used to via credit card and download your PDF document instantly.

Student with book image

“Bought, downloaded, and aced it. It really can be that simple.”

Alisha Student

Frequently asked questions