UTANGULIZI
Kwenye mchakato wa kukusanya mashairi haya, washairi kumi na mmoja wamejikusuru
kuivulia nguo fani hii na kupiga kachombe humo kuangazia masuala yanayoikabili jamii pana
walimokulia. Washairi hawa wachanga ambao walizuumu kuandika yanayowazingira kila
uchao wamedhibitisha kuwa baada ya muda mrefu na dhana kuwa ushairi ni watu wa umri
mkubwa, vijabna nao wana jukumu kubwa la kuusongesha mbele ushairi hasa wa
kimapokezi.
Vijana hawa, wavulana kwa wasichana wamevuka viunzi vya kuitwa makinda au
machipikuziki na kudhihirisha upevu wa kazi zao. Wameyashughulikia masuala
yanayowakumba wao kama wanavyoyaona kwa jicho la ujana wao, kama wanavyosikia kwa
masikio yay a ujana na wanavyohisi kwa hisia zao za ujana pasi na kushurutishwa ama
kuelekezwa na mtu ambaye hana mwanao kuhusu hisia zao. Mathalan, wameyashughulikia
mapenzi kwa undani, utamu na uchungu wake, usaliti na yote yanayoibuka pindi mapenzi
yanapotajwa. Wameuzungumzia uongozi na siasa wanavyoziona wao na kutoa mchango
wao kwa jinsi wanavyotaka mambo kuendeshwa. Wameyaeleza maudhui mengine na
masuala ibuka kwa jinsi wanavyohisi wao.
Washairi hawa walikuja pamoja kwa malengo kadha ambayo nitakuwa mkosaji iwapo
sitayaweka wazi. Mwanzo, kilichowaleta pamoja ni kukanusha dhana inayodhaniwa sana
kuwa vijana hawawezi kufanya mambo yao pamoja. Sina shaka kuwa hapa nchini hii ndio
diwani ya kwanza ambayo imewaleta pamoja vijana wengi. Kwa hilo, hatuna shaka kuwa
tumepiga hatua kubwa sana.
Pili, lililowasukuma washairi hawa ni kutoa mwelekeo wakati huu mgumu katika tasnia ya
fasihi ambapo wengi kati ya vijana wameubwagia silaha ushairi. Dhana kwamba ushairi ni
mgumu na kuwa ni fani ya wakongwe ambayo imekuwa ikiuhatarisha ushairi imechangia
pakubwa mjo wao pamoja kuikanusha kwa kinywa kipana. Diwani hii ni ithibati kwa hilo.
Wakati Sanaa nyingine zimekuwa zikipitia mabadiliko na mkengeuko mkubwa, ushairi
haukusazwa nyuma. Nao umepitia mengi hasa kwa athari za kimagharibi. Jambo hili
limekuwa si kikwazo tu bali pia mwiba mkuu katika ushairi wa kimapokeo. Ujio wa diwani hii
ni ishara tosha kuwa wapo watetezi wa ushairi wa kimapokeo ambao wamehiari kuuhisha
kwa manufaa ya kizazi cha sasa na halafu.
Waandishi hawa wamejizatiti kwa kutunga mashairi ya miundo tofauti na yenye maudhui na
dhamira tofauti. Kwa hili, sina shaka kuwa walijitolea sabili kulifanikisha. Ujumbe wenyewe
ni mpana uliokolea mafunzo, zinduo, makanyo na elimu ya kuwafanya wengi kuonoka katika
maisha ya kila siku. Haitakuwa vyema ikiwa utapitwa na tunu iliyomo katika nudhumu hizi.
Nakutakieni usomaji wenye mafanikio
Jibril Adam,
, WAANDISHI
1. Nana Martha Gaceri
2. Moses Chesire
3. Ayeko Jakoyo
4. Allan Chevukwavi
5. Brandi Msanii
6. Ramadhan Savoge
7. Okello wesonga
8. Uledi Brian
9. John wanyonyi
10. Jibril N. Adam
11. salim Abdalla Bakari
, Sura ya kwanza
ISTILAHI ZA USHAIRI
Mshororo: mshororo ni mstari mmoja katika shairi ambao hupangwa ili kueleza ujumbe
katika ubeti.
Ubeti : ubeti ni mkusanyiko wa mishororo iliyopangwa pamoja ambayo hujenga ujumbe
fulani kwa ukamilifu.
Kina : kina ni kitamkwa kinachotokea mwishoni mwa mshororo ama kijisehemu chake
ambacho hujirudia katika ubeti huo wa shairi.
Kibwagizo:kibwagizo ni mshororo unaoridiwarudiwa katika ubeti wa shairi. Pia huitwa
mkarara, kiitikio au kipokeo
Mizani: ni idadi ya vitamkwa katika mshororo ambavyo vinawezesha utosheezi wa
kukaririka kwa ubeti.
Mwanzo:huu ni mshororo wa kwanza katika ubeti wa shairi.
Mloto : huu ni mshororo wa pili katika ubeti wa shairi
Mleo : ni mshororo wa tatu katika ubeti wa shairi. Pia huitwa mlea.
Kipande: ni sehemu inayojitenga katika mshororo kama vile ukwapi,utao na mwandamo.
Hutenganishwa kwa koma (,)
Ukwapi:kipande cha kwanza katika mshororo
Utao : kipande cha pili katika mshororo
Mwandamo : kipande cha tatu katika mshororo. Pia huitwa mwandamizi.
Ukingo :kipande cha nne katika mshororo baada ya mwandamizi.
Malenga: msanii mwenye ubunifu na ujuzi wa kuyatunga mashairi.
Manju: msanii mwenye ujuzi wa kutunga na kuimba nyimbo na mashairi
Ghani:ni kuimba shairi au nyimbo yenye mapigo na urari. Pia ni faladi.
Muwala : ni mtiririko wa shairi ambao unatiririsha mawazo na kurahisisha uelewekaji wa
shairi.
, UHURU WA MSHAIRI.
Kila kazi ya kisanii ina kanuni zake. Mshairi naye piwa hajasazwa. Zipo kanuni ambazo
mshairi anapaswa kuzitumia katika ufanikishaji wa kazi yake.
1. Kuboroga sarufi
Mshairi amepewa uhuru wa kutunga kazi yake pasi na kuibana katika mikatale ya sarufi.
Asipoweza, huruhusiwa akikiuka baadhi ya kanuni za wazi za kisarufi ambazo katika kazi
nyingine za kiubunifu huwa ni kosa. Cha msingi huwa ni utoshelezaji.
Mfano, badala ya kusema Mola hakupi zaidi hupinduliwa na kuwa zaidi hakupi Mola.
2. Tabdila
Huu ni uhuru ambao katika utoshelezi wa shairi, mshairi anaweza kubadilisha sauti katika
maneno ili kuainisha maendelezo fulani pasi na kuathiri idadi ya mizani kwenye mshororo.
Mfano, sikiya badala ya sikia.
3. Inkisari
Huu ni uhuru wa kishairi ambao unamruhusu mshairi kufupisha maendelezo ya maneno
kwa kudondosha silabi ili kutimza utoshelezaji wa mishororo.
Mfano. Walosema badala ya waliosema.
4 .mazida
Huu ni uhuru wa mshairi unaowezesha urefushaji wa silabi katika mameno kwa matilaba ya
kutosheleza mizani au urari .